SOMO:KUISHI MAISHA MATAKATIFU NI KUISHI BILA KUTENDA DHAMBI - APOSTOLIC FAITH RESTORATION MINISTRY

Breaking

KILA SIKU

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday, 18 August 2017

SOMO:KUISHI MAISHA MATAKATIFU NI KUISHI BILA KUTENDA DHAMBI



Mch. Lameck Stephen.














































SOMO:KUISHI MAISHA MATAKATIFU NI KUISHI BILA KUTENDA DHAMBI
1Yohana 3:9. - Kila mtu aliyeza
liwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu. – Je, inawezekana kweli?
Yesu akamwambia, “Wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende dhambi tena” (Yoh.8:11(b)“ Watakatifu waliopo duniani ndio walio bora hao ndio niliopendezwa nao” (Zab.16:3)
Iweni watakatifu…
1. Dhambi Ni Nini?
a. Ni hali ya kukosesha utakatifu au hali ya kukoseha kuwa na haki mbele za Mungu.
2. Kutenda Dhambi ni kulitenda jambo linalosababisha ukose utakatifu au kukosa kuwa mwenye haki mbele za
Mungu.
3. Asili Ya Dhambi/Chanzo Cha Dhambi
a. Ni tamaa, ikichukua mimba huzaa dhambi, dhambi ikikomaa huzaa mauti. (Yak.1:13-15)
Aina Za Dhambi (Walawi sura ya nne; 1Yoh.5:16-18)
1. Dhambi ya mauti – ni dhambi isiyosameheka.
2. Dhambi isiyo ya mauti – Inayosameheka
3. Dhambi ya kukusudia/kuamua kuitenda; kwa sababu ya visababu unavyoviona wewe mwenyewe kuwa
vinakuhalalisha kutenda dhambi.
a. Ni kufahamu kabisa kuwa jambo fulani ni dhambi lakini unalitenda tu, eti kwa sababu wewe ni
mwanadamu si malaika, wewe ni dhaifu.
b. Kwa sababu eti una hali ngumu ya kimaisha kama umasikini, ugonjwa njaa hatari … hivyo kuiba, kuua,
kudanganya, kuzini, …
c. Kutenda lisilo haki.
d. Kufahamu kabisa kwamba kutenda jambo fulani ndiyo haki, lakini unaamua kwa makusudi kabisa
kutenda kinyume chake. Yak.4:17
e. Onyo kuhusu kutenda dhambi kwa makusudi: Ebr 10:26-31
4. Dhambi ya kutokukusudua/ kutokuamua wewe mwenyewe kuitenda; bali ni kutokana na yafuatayo (lakini si
kwa bahati mbaya; hakuna dhambi ya bahati mbaya!): -
1. Kushindwa kuiepuka Kutokana na: -
1. Kukoseshwa/kukwazwa (Mt.18:7-14) na: -
a. Ulimwengu
1. Mwanadamu mwingine
2. Matendo ya kukosesha/ kukwaza
3. Kutendewa mambo ya kukufanya uchukue uamuzi ambao ni dhambi, kama vile;
kukasirika, kutukana, kupigana, kuchukia, kuzini, kuiba … Mfano: Mafundisho,
ushawishi, Mitindo ya mavazi, mazingira …
b. Mazingira au hali ya kutoepukika.
1. Ujinga)
Kutokujua (kuwa unalolitenda ni dhambi.-Luk.12:43-48
2. Ajali
3. Kazi – askari, vitani kuua.daktari-kukosea na mgonjwa kufa; kiwanda cha
sigara/pombe.
2. Shetani - mpinzani; Ibilisi mshitaki.
i. Majaribu- ushawishi wa kutenda dhambi (jaribu siyo dhambi, bali kutii ushawishi wa jaribu ni
dhambi)
ii. Kufungwa na nguvu za giza na kutumikishwa na roho mbaya katika kazi za ibilisi; kwa
mashambulizi ya nje au ya ndani kupagawa)
iii. Kutumikishwa na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho, mfano pepo la wizi,
ulevi, uzinzi, hasira, uuaji, ujambazi, ukahaba, uchawi, maringo, kiburi, uongo, uvivu dharau,
umasikini, tamaa, …
3. Mwili.
A. Uvivu – Uzembe/ ulegevu
Kupenda starehe, raha, na faraja kuliko shida.
Hudanganya kungojea miujiza tu badala ya kufanya kazi na bila kuchukua hatua ili kutimiza wajibu wa kimwili na kiroho.
Hujenga hali ya kutaka kupokea tu badala ya kutaka kutoa.
Huleta umaskini na laana katika maisha (Yer.48:10;)
Ni usingizi wa kiroho (Mith.6:6-11)
B. Uchafu / ufisadi –Mwenendo usio mtakatifu.
C. Sauti ya ndani - Kimtokacho mtu – (Mrk.7:15-20)
Mawazo (kukumbuka/kusahau, kukubali/kukataa, kuelewa/kutoelewa, kutambua/kutokutambua, kufikiria / kutokufikiria, Mema au mabaya.)
Dhamiri / Nia / Makusudi kutaka / kutokutaka, Mema au mabaya.
Hisia, hofu, mashaka, woga, aibu, uchungu / furaha, huzuni.
Kusema maneno moyoni. (Rum.10:8-11)
Tamaa, vita katika viungo vya mwili
Aina za tamaa
1. Tamaa za Macho-Kuona na kujenga hamu ya kutaka kupata au kutenda kinyume na utaratibu wa kweli.
2. Tamaa za Mwili-Misukumo ya mwili kwa ajili ya hamu ya kutaka kupata au kutenda kinyume na utaratibu wa kweli (wa neno la Mungu) katika hamu ya :-
1. Chakula kutokana na njaa
2. Kunywa kinywaji kutokana na kiu
3. Kutaka mwenzi wa maisha kutokana na misukumo ya kijinsia (ashiki) yaani kutaka kuoa au kuolewa.
4. Makosa - Ni dhambi ya kutokukusudia.
a. Kukusudia kufanya vizuri kwa nia njema kabisa, lakini kumbe sivyo inavyotakiwa.
b. Ni kutenda tofauti na vile ilivyotarajiwa kutendeka.
1. Mfano:
a. Kuitikia wito wa Mungu isivyostahili. (Rum.10:1-4; 1Sam3:1-8)
b. Kudhania ya kuwa unampendeze Mungu kumbe unamchukiza
i. Sauli kuangamiza wakristo wa kanisa la kwanza. (Yoh.16:1-3)
ii. Binti Herodi kuomba kichwa cha Yohana Mbatizaji badala ya kuomba
kitu kizuri – maomba mabaya! (Far.18)
Heri utende halafu ukosee kuliko kutokutenda kabisa, ni kukosa utii!
Mungu huyasitiri makosa ya atubuye na kuamua kumfuata Yesu Kristo. (Zab.32:1-2)
5. Kuanguka dhambini (yaweza kuwa dhambi ya kutokukusudia au ya kukusudia)
a. Ni kuipoteza hali ya utakatifu ambayo ulikuwa nayo au kurudia hali ya dhambi wakati ulisha takaswa
hapo kwanza. (Nguruwe aliyeoshwa kurudi matopeni, au mbwa kuyarudia matapishi yake)-
b. Ni kuuacha wokovu na kuamua kuishi dhambini. Ebr.6:4-8; 2Pet. 20-22.
6. Kuishi dhambini (yaweza kuwa dhambi ya kutokukusudia kama mtu hajakutana na nuru ya neno la Mungu au ya kukusudia kama aliwahi kukutana na nuru ya neno la Mungu au wokovu)
a. Ni kuishi maisha ambayo huona kutenda dhambi ni hali ya kawaida
b. Kutokumcha Mungu; yaani bila kuona aibu au hofu ya dhambi mbele za Mungu.
c. Ni kuishi bila kujitakasa. (Mtakatifu…)
7. Uasi - Ni dhambi ya kukusudia.
a. Ni Hali ya kukiuka amri au kuto kuzitii amri au kufatonya na kutotimiza maagizo uliyopewa na
kuyafahamu kabisa, uliyoamuriwa au uliyoambiwa.
8. Chukizo (Yaweza kuwa dhambi ya kutokukusudia au ya kukusudia)
a. Ni kufanya kwa makusudi kabisa yale yasiyokubalika au yasiyompendeza Mungu; tena yaliyo
najisi.
b. Ni kufanya yaliyo maudhi ili kumkasirisha Mungu kwa nia ya kuwa kinyume na mambo ya Mungu au
kufanya upinzani.
9. Kurudi nyuma – inahusiana na utendaji wa mambo ya Mungu. (Yaweza kuwa dhambi ya kutokukusudia
au ya kukusudia)
a. Kuacha au kupunguza bidii ya utendaji wa amri, maagizo, sheria za Mungu, au neno la Mungu.
b. Ni kutokana na kukata tamaa kwa sababu ya magumu au kutokupata jibu katika maeneo
mbalimbali.(1Sam.15:10-11)
Tamaa ni hamu ya kutaka kuupendeza mwili au kutimiza matakwa ya mwili vile utakavyo
hata kama ni kinyume na mapenzi ya Mungu.
Misukumo ya mwili ni ya kawaida na si dhambi; kwani imewekwa na Mungu ili kuyatimiza
matakwa ya mwili (mahitaji / hamu) si kama utakavyo bali katika mapenzi ya Mungu
kulingana na neno lake.
Hamu au kuhitaji ni misukumo ya mwili iliyo ya kawaida kimaumbile kadiri ya uumbaji wa
Mungu na wala si dhambi ikitimizwa katika utaratibu wa Mungu kulingana na neno lake
(soma 1tim.4:1-8 )
Aliyezaliwa na mungu hatendi dhambi kwa kuwa ameamua kikwelikweli kutotenda dhambi; na Mungu
humsaidia kwa neema yake. Bali yawezekana akaingia katika dhambi ya makosa ambayo Mungu kwa
neema yake humsitiria makosa hayo na kumhesabia haki(zab.32:1-2)
Dawa ya dhambi
i. Toba ni kuuziungama dhambi na kubadilika kabisa; tena upesi bila kuchelewa.(Ebr.12:1-3)
ii. Kuoshwa / kutakaswa kwa damu ya BWANA Yesu Kristo.
iii. Kutokutenda dhambi tena.
iv. Neema ya mungu. Ipo kwa kila amwaminiye BWANA Yesu kama bwana na Mwokozi wa
maisha yake(Aliyeokoka)
v. Kulitii Neno la Mungu.
Matokeo ya dhambi
- Inaleta mafanikio ya muda mfupi lakini lazima utavuna ulichopanda katika mwili au katika roho; iwe umetubu au hukutubu.
- Inaleta laana kwako na kwa wengine wakuzungukao
- Inaleta hukumu na kifo cha kiroho.
Dhambi popote ilipo na katika chochote lazima itaadhibiwa na Mungu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here